Najiuliza: hivi tukifika Oktoba 28 na Maalim Seif bado mzima kasimama mbele yetu na kwenye kipande cha kura yumo, tutakimbilia wapi? Hivyo Kisiwandui sasa kumekuwa na Israel tu, hakuna tena akili za kupanga mikakati ya ushindi?

Jana, Leo na Kesho

Maelfu ya wakaazi wa kisiwa cha Unguja wamejitokeza leo kwenye mapokezi ya wagombea wa urais wa Zanzibar na Muungano kupitia chama cha ACT-Wazalendo – Maalim Seif Sharif Hamad na Benard Membe, sambamba na mgombea mwenza, Profesa Omar Fakih Hamad, pamoja viongozi wengine wa chama hicho. Angalia tukio zima kwa picha.
Maalim Seif Sharif Hamad, anayewania tena urais wa Zanzibar kwa mara ya sita mfululizo, aliambatana na Benard Membe anayewania urais wa Jamhuri ya Muungano akiwa na mgombea mwenza wake, Profesa Omar Fakih Hamad, pamoja na Kiongozi wa Chama Zitto Kabwe.
“Msajili hana uwezo wa kukifuta chama chetu. Sheria inamzuwia. Tena sheria hiyo ameiandika mwenyewe. Njooni kwenye ACT Wazalendo. Asiwatisheni huyu.”
Maalim Seif, ambaye kama akipitishwa atakuwa anawania nafasi hiyo kwa mara ya sita mfululizo, alisema kuchukuwa kwake fomu hiyo hakumaanishi kwamba milango imefungwa kwa wanachama wengine wenye nia ya kuwania wadhifa huo.