Khalifa Hatfar: Kibaraka wa Marekani au mwokozi wa Libya?

Published on :

Haftar anaishtumu serikali ya Tripoli kuwa imejaa magaidi na amekuwa akidai kwamba lengo lake ni kuwapiga vita magaidi wote wenye kufuata mielekeo mikali ya Kiislamu kama vile wafuasi wa Dola ya Kiislamu (Islamic State) au Al Qa‘eda.  Amekuwa akishtumu kwamba wote wenye kuingiza dini katika siasa ni magaidi wakiwa pamoja n ahata wafuasi wa vuguvugu la Udugu wa Kiislamu (Jami’yat al Ikhwan al Muslimin).

Mzanzibari ateuliwa jopo la majaji Tuzo ya Caine

Published on :

Ahmed Rajab, mwandishi wa habari wa kimataifa na mchambuzi wa masuala ya kisiasa duniani ambaye ni mzaliwa za Zanzibar, ameteuliwa kuwa mmoja wa majaji wa Tuzo ya Caine kwa Waandishi wa Kiafrika kwa mwaka 2018. Taarifa iliyotolewa na watayarishaji wa Tuzo hiyo ya kimataifa inasema Ahmed Rajab ataungana na majaji […]

‘Dystopia’ na machungu ya viongozi wakali

Published on :

NIMEKUWA nikilitafuta neno moja la Kiswahili kuielezea hali ya Zanzibar ilivyo na inavyoelekea kuwa endapo mambo yake yataendelea kuwa yayo kwa yayo, tuseme katika kipindi cha miaka kumi au ishirini ijayo.  Kila neno nililolizingatia na kulipima nimehisi kuwa halikidhi haja. Halitoshelezi kuielezea jinsi hali hiyo ilivyo au itavyokuwa katika miaka […]

Tujihadhari na “watoto wa kambo” wa Hitler

Published on :

WIKI iliyopita nilipata baruapepe kutoka kwa rafiki yangu mmoja wa Burkina Faso ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa chanda na pete na Blaise Compaoré, Rais wa nchi hiyo aliyepinduliwa kwa ghadhabu ya umma mwishoni mwa Oktoba 2014. Waburkinabé, wananchi wa Burkina Faso, walikuwa wamekwishamchoka Compaoré aliyekuwa madarakani kwa miaka 27. […]