Najiuliza: hivi tukifika Oktoba 28 na Maalim Seif bado mzima kasimama mbele yetu na kwenye kipande cha kura yumo, tutakimbilia wapi? Hivyo Kisiwandui sasa kumekuwa na Israel tu, hakuna tena akili za kupanga mikakati ya ushindi?

Jana, Leo na Kesho

Maalim Seif Sharif Hamad, anayewania tena urais wa Zanzibar kwa mara ya sita mfululizo, aliambatana na Benard Membe anayewania urais wa Jamhuri ya Muungano akiwa na mgombea mwenza wake, Profesa Omar Fakih Hamad, pamoja na Kiongozi wa Chama Zitto Kabwe.
“Msajili hana uwezo wa kukifuta chama chetu. Sheria inamzuwia. Tena sheria hiyo ameiandika mwenyewe. Njooni kwenye ACT Wazalendo. Asiwatisheni huyu.”
Viongozi wawili waandamizi wa chama cha ACT Wazalendo, Nassor Mazrui na Ismail Jussa, wamechukuwa fomu hivi leo (19 Julai) kuomba ridhaa ya chama chao kuwania uwakilishi kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.
Maalim Seif, ambaye kama akipitishwa atakuwa anawania nafasi hiyo kwa mara ya sita mfululizo, alisema kuchukuwa kwake fomu hiyo hakumaanishi kwamba milango imefungwa kwa wanachama wengine wenye nia ya kuwania wadhifa huo.