Ni aibu kwa SMZ kutomtambua mshindi wa fasihi Ali Hilal

Published on :

Yapata miaka miwili sasa tokea nipate kumjuwa Ndugu Ali Hilali Ali, nilishawishika kuomba urafiki kupitia mtandao wa ‘facebook’ kutokana na michango na elimu yake anayotoa kwa jamii kupitia ukuta wake huo, kutokana na uungwana wake mkubwa hakusita kukubali ombi langu na toka hapo tumekuwa tukiwasiliana mara kwa mara kupitia kuta […]

Baina ya mkandarasi na kandarasi

Published on :

Mmojawapo miongoni mwa washairi maarufu wa Tanzania, Khamis Amani Nyamaume (1926-1971), katika shairi lake labeti nne, liitwalo ‘Saa’, alitunga akasema: Saa za huku na huko, zimekosana majira Sababu ni mzunguko, haufuati duara Sasa rai iliyoko, ni kubadilisha dira Saa zatupa majira, mafundi zitengezeni…

N’na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini

Published on :

Siku ilikuwa Jumatano. Tarehe ilikuwa 1 Septemba 2010. Majira yalikuwa ya saa 4:00 usiku. Mahala palikuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam, mji mkuu wa kibiashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nakumbuka kila kitu kuhusu siku hiyo. Nikiwa kwenye sehemu ya kusafiria […]

Dunia kokwa ya furu: Amali ya Misemo ya KiPemba

Published on :

Jitihada za ukusanyaji na uchambuzi wa data za kifoklo za launi za Kipemba si jambo geni (angalia Whiteley (1958) na Mlacha (1995:21-25). Lakini kadri, muda unavyopita jitihada hizo zinaelekea kupungua kasi. Suala la uhifadhi wa ‘bohari la hekima ya wahenga wetu kimaandishi’ ni la wajibu na halipaswi kusita. Katika mradi […]

Uhusiano baina ya Kimakunduchi na Kiswahili Sanifu

Published on :

Kumekuwa na mjadala mrefu miongoni mwa wataalamu wa lugha ya Kiswahili ikiwa kile kichachoitwa Kiswahili Sanifu ni lugha kamili na tafauti na lugha nyengine zinazozungumzwa kwenye maeneo yanayopakana nacho, kama vile Kimakunduchi (au Kikaye) kinachozungumzwa kusini mwa kisiwa cha Unguja, au zote kwa pamoja ni lahaja za lugha moja kuu, […]