Katika hatua inayoonesha bado wana imani naye licha ya kuwania urais mara kadhaa na kushindwa kuingia madarakani, wanachama na wafuasi wa Chama cha ACT-Wazalendo wa Micheweni kisiwani Pemba wameamua kumchangia Maalim Seif Sharif Hamad kuwania tena urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Maalim Seif, ambaye ni mwenyekiti wa taifa wa ACT-Wazalendo amewahi kuwania nafasi hiyo mara tano mfululizo na hivi karibuni alitangaza azma yake ya kuomba tena ridhaa ya wanachama wa chama chake kuwawakilisha kwa mara nyengine tena katika kinyangànyiro hicho.Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.