Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetangaza vituo vya uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu yakiwa maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Taarifa ya ZEC kwa vyombo vya habari inasema kuwa ingeendesha uandikishaji wa wapigakura wapya na uhakiki wa taarifa za wapigakura ambao tayari wamo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa shehia zote za Wilaya ya Magharibi B na shehia za Jimbo la Tunguu kwa Wilaya ya Kati kuanzia tarehe 25 Februari hadi 29 Februari mwaka huu.

ZEC imewataka wale wanaokwenda kujiandikisha kuhakikisha kuwa wana vitambulisho vyao vya Mzanzibari Mkaazi na wale wanaohakiki taarifa zao wawe na vitambulisho vya kura na vya Mzanzibari Mkaazi kwa pamoja.

Kwa mujibu wa Tume hiyo, vituo vyote vitakuwa vikifunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni, huku ikionya kwamba ni lazima kwa kila mtu anayetaka kuwa mpigakura kwenda mwenyewe kituoni na sio kutuma mtu wa kumuwakilisha.

Angalia ratiba kamili hapa:

JIMBO LA MWANAKWEREKWE

 • Wananchi wa Shehia ya Magogoni watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Viwanda Vidogo Vidogo
 • Wananchi wa Shehia ya Mikarafuuni watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Magogoni
 • Wananchi wa Shehia ya Jitimai watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Mwanakwerekwe B
 • Wananchi wa Shehia ya Sokoni watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Urafiki Mwanakwerekwe
 • Wananchi wa Shehia ya Mwanakwerekwe watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Mwanakwerekwe A

JIMBO LA PANGAWE

 • Wananchi wa Shehia ya Mwembe Majogoo watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Msingi kinuni
 • Wananchi wa Shehia ya Mnarani watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Trifonia
 • Wananchi wa Shehia Kinuni watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Sekondari Kinuni
 • Wananchi wa Shehia ya Pangawe watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya kijitoupel

JIMBO LA KIJITOUPELE

 • Wananchi wa Shehia ya melinne watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Sekondari Mwanakwerekwe C
 • Wananchi wa Shehia ya Taveta watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Mbarali Meli Nne
 • Wananchi wa Shehia ya Uzi watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Uwanja wa Magirisi
 • Wananchi wa Shehia ya Kijitoupele watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Tanwiir

JIMBO LA FUONI

 • Wananchi wa Shehia ya Fuoni Kipungani watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Raudha Academic Kituo A
 • Wananchi wa Fuoni Migombani watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Raudha Academic Kituo B
 • Wananchi wa Shehia ya Mambosasa watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Mambosasa
 • Wananchi wa Shehia ya Chunga Watajiandikisha na kuhakiki taaarifa zao katika kituo cha Skuli ya Msingi Chunga na Skuli ya Msingi Fuoni

JIMBO LA DIMANI

 • Wananchi wa Shehia ya Fumba watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Maandalizi Fumba
 • Wananchi wa Shehia ya Bweleo watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya maandalizi Bweleo
 • Wananchi wa Shehia ya Dimani Watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Dimani
 • Wananchi wa Shehia ya Kombeni watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Kombeni na Skuli ya Maandalizi Kisakasaka
 • Wananchi wa Shehia ya Nyamanzi watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Maandalizi Nyamanzi
 • Wananchi wa Shehia ya Maungani watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Maungani
 • Wananchi wa Shehia ya Uwandani watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Skuli ya Sekondari Fuoni
 • Wananchi wa Shehia ya Kibondeni watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Kibondeni na Skuli ya Kibonde Mzungu
 •  
 • JIMBO LA CHUKWANI
 • Wananchi wa Shehia ya Kisauni watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Kisauni
 • Wananchi wa Shehia ya Tomondo watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Skuli ya Biashara
 • Wananchi wa Shehia ya Shakani watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Maandalizi Shakani
 • Wananchi wa Shehia ya Chukwani watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Chukwani na Chuo cha Ufundi Karume

JIMBO LA MWERA KIEMBE SAMAKI

 • Wananchi wa Shehia ya Kiembe Samaki watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Msingi Kiembe Samaki A
 • Wananchi wa Shehia ya Michungwani Watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Kiembe Samaki B
 • Wananchi wa Shehia ya Mbweni watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Kiwanda cha Usumba Mbweni
 • Wananchi wa Shehia ya Mombasa watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya SOS
 • Wananchi wa Shehia ya Kwamchina watajiandikisha na kuhakiki taarifa zake katika kituo cha Uwanja wa Mpira Kwamchina

WILAYA YA KATI JIMBO LA TUNGUU

 • Wananchi wa Shehia ya Ubago watajiandikisha na kuhakiki taarifa za katika kituo cha Skuli ya Ubago, Skuli ya Mwera na Skuli ya Mwera Pongwe
 • Wananchi wa Shehia ya Dunga Bweni watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Maandalizi Dunga Bweni
 • Wananchi wa Shehia ya Dunga Kiembeni watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Msingi Dunga Kiembeni
 • Wananchi wa Shehia ya Binguni watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Maandalizi Binguni
 • Wananchi wa Shehia ya Tunguu watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Tunguu na Skuli ya Kibele
 • Wananchi wa Shehia ya Jumbi watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Jumbi
 • Wananchi wa Shehia ya Bungi watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Bungi
 • Wananchi wa Shehia ya Kikungwi watajiandikisha na kuhakiki zao katika kituo cha Skuli ya Kikungwi
 • Wananchi wa Shehia ya Unguja Ukuu Kaebona watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Unguja Ukuu
 • Wananchi wa Shehia ya Tindini watajiandikisha na kuhakiki zao katika kituo cha Skuli ya Maandalizi Tindini
 • Wananchi wa Shehia ya Unguja Ukuu Kaepwani watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Maandalizi Kaepwani
 • Wananchi wa Shehia ya Uzi watajiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika kituo cha Skuli ya Uzi
 • Wananchi wa Shehia ya Uzi Ng’ambwa watajiandikisha na kuhakiki katika kituo cha Skuli ya Maandalizi Ng’ambwa

 

 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.