Mchezaji bingwa wa ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani (NBA), Kobe Bryant, amefariki dunia baada ya helikopta aliyokuwa akisafiria kuanguka Los Angeles.

Bryant, aliyekuwa na umri wa miaka 41, alipata ajali hiyo siku ya Jumapili (Januari 26) akiwa na watu wengine wanne kwenye helikopta hiyo ya binafsi.

Ofisi ya Mkuu wa Kaunti ya Los Angeles ilituma ujumbe wa Twitter ikithibitisha kuwa watu wote watano waliokuwemo kwenye helikopta hiyo walipoteza maisha.

Bryant alikuwa mchezaji wa kwanza mpira wa kikapu nchini Marekani kutunukiwa tuzo ya filamu ya Academy Award mwaka 2018 kwa filamu fupi ya michoro iitwayo “Dear Basketball”.

Mchezaji huyo mwenye asili ya Afrika amewacha kizuka na watoto wanne.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.