Bei ya mafuta yapanda baada ya mashambulio dhidi ya vituo vya mafuta nchini Saudia.

Gharama ya mafuta imepanda kwa kiwango cha juu kuwahi kushuhudiwa katika miezi minne baada ya mashambulio mawili dhidi ya vituo vya mafuta Saudi Arabia Jumamosi yaliosababisha kumwagika kwa 5% ya mafuta duniani.

Kiwango cha mafuta ghafi yalipanda kwa 19% kwa thamani ya $71.95 kila mtungi huku viwango vingine, West Texas Intermediate, vikipanda 15% kwa thamani ya $63.34.

Bei zilishuka kidogo baada ya rais wa Marekani Donald Trump kuagiza kufunguliwa kwa akiba nchini Marekani.

Mashambulio hayo dhidi ya vinu katika shina la viwanda vya mafuta saudia vinajumuisha kituo kikubwa duniani cha usafishaji mafuta.

Fire at Saudi oil facility

Waziri wa nishati mwanamfalme Abdulaziz bin Salman amesema kupungua kwa utengenezaji mafuta kutafidiwa kwa kutumia akiba kubwa iliopo.

Hatahivyo, Michael Tran, mkurugenzi msimamizi wa mipango ya nishati katika soko la RBC Capital Markets mjini New York, amesema: “hata iwapo tatizo hilo litatatukiwa kwa haraka, tishio la kutenga 6% ya mafuta yanayotengenezwa duniani sio fikra tu. Kutahitajika, faida ya ziada inayohitajika kwa mwekezaji kujilipa.”

Saudi Arabia with capital Riyadh, the two oil facilities Abqaiq and Khurais, Yemen to the south and Iraq and Iran to the north

Bwana Pompeo amesema Tehran imehusika na mashambulio hayo ya uharibifu lakini hakutoa ushahidi maalum kuunga mkono tuhuma zake.

Amepinga tuhuma za waasi wa Houthi nchini Yemen wanaoungwa mkono na Iran kwamba wao ndio waliotekeleza mashambulio hayo.

Iran imeishutumua Marekani kwa ‘uongo’ na waziri wake wa mambo ya nje Javad Zarif amesema kuwa “kuituhumu Iran hakutomaliza janga” nchini Yemen.

chanzo: BBC swahili

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.