Familia ya Mugabe ambaye alifariki Singapore wiki iliyopita, na serikali ya Zimbabwe wamekuwa wakizozana juu ya mahali utakapozikwa mwili wake.

Mzozano huo ni juu ya ikiwa kiongozi huyo wa zamani, atazikwa katika kijiji chake cha Kutama kilichoko Kaskazini magharibi mwa Harare au katika makaburi ya mashujaa yalioko pia mjini Harare

Mapema hivi leo rais wa sasa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza kuwa mwili wa rais wa zamani Robert Mugabe utazikwa katika makaburi ya taifa ya mashujaa wa ukombozi kama ilivyo ada na desturi.

Hatahivyo familia ya rais wa zamani Robert Mugabe, imesema mwili wa kiongozi huyo utazikwa mapema wiki ijayo kijijini kwake na sio katika makaburi ya taifa ya mashujaa wa ukombozi.

Chanzo: Dw Swahili.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.