Je unajua kwamba baadhi ya viungo vya maiti vinaweza kuwa msaada katika matibabu ya wagonjwa wengine walio hai?

Kampeni mpya imeanzishwa nchini Tanzania kuhamasisha na kutoa wito kwa wananchi kuruhusu baadhi ya viungo vya ndugu zao waliofariki kuchukuliwa ili visaidie wengine walio na uhitaji wa viungo hivyo.

Ni kutokana na uhaba huu ndio kampeni imeidhinishwa kuelimisha wananchi kusudi angalau waweze kusaidia kuibadili hali na kuwasaidia wengine.

Aidha Dkt Joseph anafananisha mchakato huo na utoaji damu ambao kampeni na uhamasishaji mkubwa umefanyika na kuwafanya watu kuchangia damu ‘kwa ajili ya kuweza kuwasaidia ndugu ambao watakuwa na matatizo’.

organ

Baada ya mtu kufariki kuna muda ambao viungo bado viko hai baada ya mtu roho kutoka. katika muda huo ambapo vikiwahi kutolewa na vinaweza kusaidia watu wengine walio hai katika upasuaji wa upandikizaji wa viungo kama inavyofanyika katika matiafa ya Ulaya na hata India.

Hali hioyo kwa sasa ni kwamba hakuna malipo yanayotolewa kwa utoaji huo wa viungo ni kama uchangiaji damu ambao hufanyika kwa uhisani tu wa mtu binfasi.

aktari anafafanua kuwa kuna .

Viungo maalum vinavyolengwa Mfano Moyo , figo au kioo cha jicho ndio viungo vyenye uhitaji mkubwana hutumika katika upandikizaji kuwasaidia wagonjwa.

Hatahivyo hali hii inatiliwa shaka na baadhi ya watanzania kwa kutokuwa na uaminu na jambo hilo. Wengi wanahofia kujitolea viungo vya watu na kufanywa biashara. wengine wamesema kuwa hawaweezi kuchangia kutokana na imani za dini yao na baadhi yao kusema kuwa marehemu ana heshima yake japo kuwa amekufa na kutoa viungo vyake ni kama kumkashifu.

chanzo: BBC swahili

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.