Maoni mgawanyiko yaliyotolewa kumuhus Robert Mugabe alipokuwa hai, hayabadilika hata baada ya mauti yake . Wazimbabwe wanakumbuka kuhusu ni nini alichowaachia kiongozi huyo aliyeiongoza Zimbabwe kwa miaka 37.

Wakitumia #RIPMugabe ama #LALAsalama baadhi wanamsifu ama shujaa, mtetezi wa hadi ya watu weusi, huku wengine wakisema alikuwa mkombozi aliyegeuka kuwa mkandamizaji . Wakili wa Zimbabwe , mwanaharakati na mkosoaji wa serikali ya chama cha Zanu-PF , Fadzayi Mahere, anatafakari maoni tofauti kumuhusu namna Bwana Mugabe atakavyokumbukwa.

View image on Twitter

Baadhi ya jumbe za Twitter zilizolenga namna Mugabe atakavyokumbukwa kwa uchumi wake ambao uliathiri kila sekta ya maisha , hususan huduma za matibabu

Kwamba Bwana Mugabe – Mpigania haki za Waafrika aliyekuwa mstari wa mbele – mara kwa mara amekuwa akipata matibabu nchini Singapore na amefariki katika nchi ya kigeni ni kitu ambacho hakitasahaulika miongoni mwa wengi.

Baadhi ya Wazimbabwe pia wanatafakari juu ya kile ambacho kingetokea .Bwana Mugabe alichukua uongozi wa kitaifa akitoa ahadi nyingi nzuri mwaka 1980 alipokuwa Waziri Mkuu wa kwanza. Awali katika kazi yake ya kuleta maridhiano na kuiendeleza Zimbabwe, lakini kazi yake yote nzuri iliharibika alipoanza kampeni ya kuwatesa wapinzani na kujilimbikizia mali binafsi na familia yake.

Kwa baadhi hata hivyo, hakuna kitu kitakachoindoa thamani yamazuri aliyoyaacha Bwana Mugabe na kwamba atakumbukwa kama mkombozi dhidi ya mamlaka ya wakoloni na serikali za magharibi.

Chanzo: BBC swahili.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.