Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza amelikubali pendekezo la waziri mkuu Boris Johnson anaetaka bunge la nchi hiyo lifungwe kwa muda kuanzia kati kati ya mwezi unaokuja wa Septemba hadi kati kati ya mwezi wa Octoba.

Aidha Baraza la washauri wa malkia limesema katika taarifa yake kipindi hicho cha kusita shughuli za bunge kitaanza sio “kabla ya jumatatu inayokuja” na wala sio baada ya Alkhamisi ya september 12 kufikia jumatatu ya October 14 mwaka huu wa 2019.

Hatahivyo Waziri mkuu Boris Johnson alituma pendekezo hilo mapema hii leo kwa kile ambacho viongozi wa upinzani wanakitaja kuwa njama ya kutaka kuwazuwia wabunge kuupinga mpango wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya bila ya maridhiano.

chanzo: DW swahili

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.