Wakimbizi wa Burundi

Serikali ya Tanzania imeagiza wakimbizi kutoka nchini Burundi kurudishwa makwao, na kusema kua hali ya kiusalama katika taifa hilo sasa imeimarika.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Kangi Lugola ametangaza kuwa wakimbizi 2,000 watarudishwa Burundi kufikia October mosi.

Kangi Lugola
Image captionWaziri wa Mambio ya ndani wa Tanzania, Kangi Lugola

Mashauriano ya wakimbizi wa Burundi kurejeshwa makwao yamekuwa yakiendelea kati ya Mataifa hayo mawili na shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na Burundi imekuwa ikiiomba Tanzania kuwaachilia wakimbizi wake warudi nyumbani kulijenga taifa lao.

Aidha Bw. Lugola anadai kuwa shirika hilo la wakimbizi lina ajenda ya siri kwasababu linaleta kisingizio ambacho sio cha kweli.

Mbali na maelezo iliyopata kutoka wizara ya Mambo ya nje ya Burundi kwamba nchi hiyo ni salama waziri Lugola anasema kuwa imeridhisha kuwa wakimbizi hao watakuwa salama wakirudi makwao kwa sababu tangu mwaka 2015 hakuna hata mkimbizi mmoja aliyeingia nchini humo kutoka Burundi kwa kuhofia usalama.

Wakimbizi wa Burundi
Image captionWakimbizi wa Burundi

Mvutano kati ya shirika hilo la wakimbizi la Umoja wa mataifa na serikali ya Tanzania kuhusu suala la kuwaregesha makwao wakimbizi wa Burundi umekuwa ukiendelea kwa miaka kadhaa sasa.

Hata hivyo Serikali ya Tanzania imesifiwa kwa kuendelea kubeba mzigo huu mkubwa wa wakimbizi lakini zaidi kwa kukubali kutekeleza mkakati wa kimataifa ujulikanao kama Comprehensive Refugee Response. Ni mkakati uliolenga kutafuta namna endelevu ya kuwasaidia wakimbizi kupata ulinzi na mahitaji mengine ya msingi ya kibinadamu.

Tanzania ndio nchi inayohifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi kuliko nchi nyingine yoyote ile katika ukanda wa Afrika Mashariki

chanzo:BBC swahili

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.