Inter Milan imekubali mkataba wa mkopo kwa uhamisho wa mchezaji wa kiungo wa mbele Alexis Sanchez kutoka Manchester United.

Mkuu wa Inter Antonio Conte ana hamu ya kumsajili Sanchez kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya Jumatatu.

Iwapo makubaliano yatakamilishwa , Sanchez atajumuika na aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Man United Romelu Lukaku, mshambuliaji aliyejiunga na klabu hiyo ya Serie A kwa £74m msimu huu wa joto.

Hatahivyo, Inter haijakubali kumnunua Sanchez mwishoni mwa makubaliano hayo ya mkopo.

Mchezaji huyo anayelipwa pakubwa Man United inadhaniwa anapokea takriban £400,000 kwa wiki, kiwango kinachopita kwa ukubwa gharama ya malipo Inter .

Ilipendekezwa United inaweza kupunguza mshahara wake kama sehemu ya makhbaliano na wiki iliyopita Inter ilipendekeza kulipa £150,000 ya malipo kwa wiki ya Sanchez lakini United ilitaka fedha zaidi.

Sanchez amekuwa na kipindi kigumu cha mwaka mmoja unusu Old Trafford tangu aondoke Emirates Stadium Januari 2018, kwa kufanikiwa kufunga mara tano tu katika mechi 45.

Alifunga mara mbili msimu uliopita katika ligi kuu England na huenda angesalia katika klabu hiyo angecheza oakubwa katika ligi ya Uropa na kombe la Carabao.

chanzo: BBC swahili

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.