Unaposikia taarifa kuhusu hujuma za Acid… yaani watu kumuwagiwa tindikali usoni au Mwili mara nyingi ukatili huu huhusishwa na bara Asia. Hata hivyo kuna visa vingi vya watu kushambuliwa kwa tindikali ambavyo vinaripotiwa miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.

Mmoja wa waathiriwa ni Flavia Naampima nchini Uganda ambaye anasema alishambuliwa alipokuwa nje ya lango la nyumbani kwao alipokuwa akitoka shuleni

Ni kisa ambacho hatakisahau maishani mwake, kutokana na kwamba kilibadilisha masiha yake na anasema kila siku hupata msukumo wa kukubali kilichomtendekea miaka kumi na moja iliyopita.

Aidha ,ukatili huu husababisha thari za kisakolojia, kiakili na majeraha kutokana na hujuma za tindikali hufanya uponaji kwa manusura kuwa mgumu, kwa baadhi yao hupata changamoto kupata kazi, hivyo hulazimika kutegemea ujuzi walionao kukidhi maisha kama anavyofanya Namuyomba Jamida , anayesuka mikeka.

” Baada ya kushambuliwa kwa tindikali, maisha huwa magumu, nilipoteza kazi yangu kwa hiyo niliamua kuja mjini na hapo nilikutana na manusura wa mashambulio ya tindikali ,na kwa pamoja tukajifunza kujikimu kimaisha. Kila siku nafanya kazi hii kwa ajili ya watoto wangu watano.”

Manusura wa mashambulio ya tindikali Uganda wazungumza

Wanaharaki nchini Uganda wanahamashisha raia kuhusu ukatili huu. Reenah Ntoreinwe kutoka shirika la End Acid Violence Uganda ambalo limewasajiri manusura 350 jijini kampala pekee ana anasema sharia ni hafifu:

kulingana na takwimu katika hospitali moja jijini Kampala, katika muda wa wiki mbili hapakosi mtu aliyeshambuliwa na tindikali , jambo ambalo naibu mkuu wa polisi nchini Uganda Pauline Amaye anasema ni tatizo kubwa.

Namuyomba Jamida alikosa kazi ya kufanya na kuamua kusuka mikeka na vikapu baada ya shambulio la tindikali
Image captionNamuyomba Jamida alikosa kazi ya kufanya na kuamua kusuka mikeka na vikapu baada ya shambulio la tindikali

Daktari Adan Abdullahi anasema kwamba njia ya uponaji inachukua muda, lakini kwa matibabu yanayofaa mtu anaweza kupona kikamilifu:

Mtu anaposhambuliwa, kwanza kabisa aoshwe na maji mengi kupunguza makali. Amwagiwe maji kwa takriban dakika arobaini na tano…Tumia maji masafi kupunguza kuambukizwa kwa magonjwa kisha mgonjwa akimbizwe hospitalini katika kitengo kinachokabiliana na majeraha ya kuungua, na baada ya majeraha kupona tunaweza kufanya upasuaji wa kupandikiza ngozi upya na kurejesha umbo la muathiriwa karibu na hali ya kawaida, kando na upasuaji, matababu ya kisaikolojia ni muhimu .

Wakati Flavia na Jamida wanaendelea kupona, watu waliowashambulia waathiriwa hawajawahi kubainika na kufikishwa mbele ya sheria, na hadi pale kutakuwa na sharia kali, waathiriwa watazidi kuishi kwa hofu.

chanzo: bbc swahili

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.