Skip to content

Rais Magufuli akabidhiwa Uenyekiti wa nchi za jumuiya ya SADC



Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli leo amekabidhiwa Uenyekiti wa nchi za jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC. Magufuli amempokea Rais wa Namibia Dk.Hage Geingob alioutumikia wadhfa huo kwa muda wa mwaka mmoja.

Akizungumza mbele ya wakuu wa nchi na viongozi wa Serikali kutoka nchi 16, za jumuiya hiyo Mwenyekiti huyo mpya amesema umefika wakati kwa jumuiya za kimataifa kuiondolea vikwazo Zimbabwe kwani madhara yake si kwa nchi hiyo pekee bali pia ni kwa nchi nyingine za Afrika. Magufuli amezitaka nchi zinazounda Jumuiya ya SADC kuwa na kauli moja katika kukabiliana na changamoto zinazoikumba jumuiya hiyo ikiwemo hali ya umasikini kwa wananchi wake.

Viongozi pia wanatarajiwa kujadili masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na Usalama katikakanda ya Kusini mwa Afrika na uchimi wake. Mkutano wa leo inaadhimisha miaka 17 kubuniwa kwa Jumuiya ya maendeleo ya matifa ya kusini mwa Afrika

chanzo: DW /bbc swahili



Leave a Reply