Chanjo ya kuwakinga watu dhidi ya magonjwa ya zinaa imepita uchunguzi wa kwanza wa kiusalama. Ni ya kwanza kupita majaribio kwa binadamu.

Wataalamu wanasema chanjo hiyo ndio njia bora ya kukabiliana na ugonjwa wa Chlamydia ambao unachangia karibu ya nusu ya maambukizi ya magonjwa yote ya zinaa Uingereza.

Uchunguzi zaidi unapendekezwa kufanywa ili kubaini jinsi chanjo hiyo inavyofanya kazi na itolewe kwa kiwango gani, linasema jarida la Lancet la magonjwa ya kuambukiza.

Majaribio hayo yatachukua miaka kadhaa kubainishwa lakini kwa sasa wataalamu wanapendekeza njia bora zaidi ya kijikinga na maambukizi ya chlamydia ni kutumia mipira ya kondomu.

Chlamydia Ni ugonjwa uanaoambukizwa kupitia bakteria inayomuingia mtu anayefanya ngono bila kinga( hata bila kumuingilia mtu).

Bakteria ya Chlamydia huishi katika mazingira ya maji maji inayopatikana kwenye manii ya wanaume na katika sehemu ya siri ya mwanamke.

Mara nyingi mtu aliyeambukizwa haoneshi dalili zozote na dio sababu watu huutaja ugonjwa huo kuwa ugonjwa wa “siri”.

Usipotibiwa kwa kutumia antibiotiki, unaweza kusababisha madhara makubwa yatakayathiri kizazi cha muathiriwa.

Watu walio chini ya miaka 25 ambao wanapendelea kufanya ngono wanashauriwa kufanya vipimo vya chlamydia kila mwaka.

Huduma ya afya ya kitaifa NHS nchini Uingereza inatoa huduma ya uchunguzi bila malipo.

Watu pia wanaweza kujifanyia uchungizi binafsi kwa kununua vifaa maalum vilivyoidhinishwa kutoka kwa maduka ya kuuza dawa.

Mchunguzi Prof Robin Shattock alisema: “Matokea yalikua ya kuridhisha kwa sababu inaonesha chanjo hii ni salama na inatoa ulinzi ambao huenda ukakabiliana na maambukizi dhidi ya ugonjwa wa chlamydia.

chanzo: bbc swahili.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.