Real Madrid imeanza mazungumzo na Paris Saint-Germain kuhusu mpango wa kumsajili mshambuliaji nyota wa Brazil, Neymar. (Sky Sports)

Azma ya Barcelona kumsajili tena Neymar inategemea ikiwa klabu hiyo itamuuza Philippe Coutinho ambaye pia ni mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Brazil. (Goal)

Manchester United wako tayari kulipa £81m ambayo itawawezesha kumnyakua mshambuliaji wa Uhispania na Athletic Bilbao Inaki Williams, 25. (El Chiringuito TV – via Mail)

Pendekezo la Leroy Sane kuhamia Bayern Munich kutoka Manchester City limeathiriwa na jeraha la goti linalomkabili nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Mail)

Leroy Sane
Image captionLeroy Sane (Kulia)

Beki wa Chelsea Mbrazil David Luiz, 32, ataruhusiwa kujiunga na Arsenal kwa £8m tu. (Mirror)

Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha,26, amewasilisha ombi la kutaka uhamisho huku kukiwa na tetesi kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast akipingiwa upatu kuhamia Everton. (Express)

Palace wameiambia Everton hawatakubali kupokea chini £100m kumwachilia mshambuliaji huyof. (Guardian)

Wilfried Zaha

Everton wanatarajiwa kuwasajili beki waChelsea na kiungo wa kimataifa wa England wa wachezaji wa chinii ya miaka 21 Fikayo Tomori, 21, na beki wa kati wa Bournemouth Mholanzi Nathan Ake, 24. (Sun)

Newcastle wanakaribia kumsajili beki wa kulia – na nyuma Mswidi Emil Krafth, 25, kutoka klabu ya Ufaransa ya Amiens. (Newcastle Chronicle)

Burnley wamewasilisha ombi la dakika ya mwisho kumsaini kiungo wa kati Danny Drinkwater, 29, kwa mkopo kutoka Chelsea. (Mail)

Danny Drinkwater

Tottenham wanakaribia pia kumsaini bekki wa kushoto wa Fulham Ryan Sessegnon, 19. (Mirror)

Atletico Madrid wanajiandaa kumsajili mchezajiwa safu ya kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Independent)

Kingo wa kati wa Juventus Sami Khedira, 32, amekataa uwezekano wa uhamisho mara mbili kwa sababu anaazimia kujiunga na Arsenal. (Star)

Sami Khedira
Image captionSami Khedira, kiungo wa kati wa Juventus

Wolves wamesitisha mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 25. (Express & Star – via Daily Echo)

Robert Lewandowski ametoa wito kwa Bayern Munich kuwasajili wachezaji watatu wapya.

Mshambuliaji huyo wa Poland anataka kuimarishwa kwa safu ya mashambulizi baada ya wachezaji nyota kuhama klabu hiyo. (Goal)

Robert Lewandowski
Image captionRobert Lewandowski

Tetesi Bora Jumatano

Tottenham wamefikia makubaliano na Juventus kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, kwa dau la karibu £62m. (Sky Sports Italia, via Daily Mail)

Dybala anajiandaa kuanza mazungumzo ya mkataba na Tottenham kabla ya Alhamisi ambao ni muda wa mwisho uliowekwa kwa uhamisho wa wachezaji kukamilika. (Goal)

Paulo Dybala
Image captionPaulo Dybala

Tottenham pia wanapania kumsaini mshambuliaji wa Barcelona wa miaka 27- Mbrazil Philippe Coutinho. (ESPN)

Manchester United wameongeza juhudi ya kufikia mkataba na na kiungo wa kati Tottenham Christian Eriksen, 27. (Telegraph)

Eriksen hayuko katika mpango wa wa muda mrefu wa kocha Mauricio Pochettino, Tottenham – na tayari amethibitisha kuwa anataka changamoto mpya. (Mirror)

Mauricio Pochettino
Image captionMauricio Pochettino, kocha wa Tottenham

Uamuzi wa dakika za mwisho wa United kumhusu Eriksen unakuja licha ya tetesi ikiwa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, ataendelea kuwa katika klabu hiyo hadi mwisho wa dirisha la uhamisho litakapofungwa.

Chanzo: BBC Swahili

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.