Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan aliwaita tumbili wajumbe wa Afrika katika Umoja wa Mataifa UN mwaka 1971 wakati alipokuwa gavana wa Jimbo la California katika ukanda wa sauti uliochapishwa na The Atlantic.

Alitoa matamshi hayo ya kibaguzi katika mawasiliano ya simu kwa aliyekuwa wakati huo rais wa Marekani Richard Nixon ambaye alirekodi simu zake zote.

Gavana huyo alikasirishwa kwamba wajumbe wa Afrika katika Umoja wa Mataifa UN hawakuiunga mkono Marekani katika kura ya kuitambua China na kuipiga marufuku Taiwan.

Baada ya kura hiyo, wajumbe wa Tanzania walikuwa wameanza kucheza densi katika ukumbi wa UN.

Umoja wa mataifa

Wakati Reagan alipompigia simu bwana Nixon siku iliofuata alimuuliza iwapo alikuwa ameshuhudia kura hiyo katika runinga.

Halafu akasema: Kuwaona hao ‘tumbili’ kutoka mataifa ya Afrika, bado hawafurahii kuvaa viatu! Matamshi hayo yalimfanya bwana Nixon kucheka.

Sauti hiyo ilifichuliwa na Tim Naftali, Profesa wa Historia katika chuo kikuu cha New York, ambaye alikuwa mwelekezi katika maktaba ya rais Nixon ambayo ilihifadhi kanda zote zilizorekodiwa za rais huyo kutoka 2007 hadi 2011.

Rais Reagan aliwaita wajumbe wa marekani 'tumbili'

Akizungumza katika Atlantic, Naftali anaelezea kwamba ,matamshi hayo ya kibaguzi yaliondolewa katika mawasiliano wakati kanda hiyo ilipotolewa 2000 na makavazi ya kitaifa kwa sababu za faragha-wakati rais Reagan bado alikuwa hai.

Naftali anasema kwamba kufuatia agizo la mahakama, kanda hiyo ilichunguzwa: Kifo cha Reagan 2004 kiliondoa wasiwasi huo wa faragha.

”Mwaka jana kama mtafiti, niliomba kwamba mawasiliano yaliomuhusisha Reagan yachunguzwe upya na wiki mbili zilizopita, makavazi hayo yalitoa uknada huo mzima wa mawasiliano hayo ya 1971 yaliomuhusisha Reagan”.

Aliyekuwa rais wa Markani Richard Nixon

Kulingana na Naftali Bwana Reagan alikuwa amempigia simu rais Nixon ili kumshinikiza kujiondoa katika Umoja wa Mataifa UN, lakini katika mawasiliano hayo na rais, malalamishi ya bwana Reagan yalidaiwa kutokana na Waafrika hao.

Katika mojawapo ya mazungumzo yake na waziri wake wa maswala ya kigeni Bwana Nixon alinukuliwa akisema: Aliwaona hawa wala watu katika runinga usiku uliopita, na alisema Yesu , hawana hata viatu, na hapa, Marekani itatoa hatma yake kwa hilo….

Bwana Naftali anasema kwamba sauti hiyo inatoa mwangaza kuhusu jinsi Bwana Reagan alivyoyatetea mataifa ya ubaguzi wa rangi ya Rhodesia na Afrika kusini baadaye miaka ya 70.

chanzo:bbc

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.