Wanafunzi wapatao 50 wa shule ya sekondari katika wilaya ya mbale Mbale magharibi mwa Uganda wamelazwa hospitalini baada ya kuvuta hewa ya gesi za kutoa machozi, limeripoti gazeti la kibinafsi nchini humo, The monitor.

Wanafunzi hao walihusika katika mapigano yaliyoijbuka baina ya shule za sekondari za Mbale Secondary school na Mbale High school kutokana na uhusiano wa kimapenzi.

Inadaiwa kuwa wakati wa ghasia hizo , polisi waliamua kufyatua mabomu ya kutoa machozi katika shule ya sekondari ya Mbale yaliyowaacha wanafunzi na waalimu wao wakikimbia kwa ajili ya usalama wao.

Wanafunzi waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mbale , Joy Hospice, Viena Clinic, Mbale general clinic, miongoni mwa hospitali nyingine, limeeleza gazeti la The monitor.

Wanafunzi waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya Mbale wanasema, mapigano hayo yaliibuka baada ya mwanafunzi kutoka shule ya sekondari ya Mbale kumvamia mwanafunzi wa Mbale high school, akimshutumu kumpenda mpenzi wake wa siku nyingi.

Msemaji wa kanda ya Elgon , Bwana Robert Tukei amethibitisha tukio hilo lakini alipuuzilia mbali madai kuwa wanafunzi walilazwa kutokana na kuvuta hewa ya mabomu ya kutoa machozi.

“Polisi waliingilia kati kusitisha mapigano, yaliyokuwa yamezuka. Kama baadhi yao walijeruhiwa wakati wa mapigano, si lazima iwe ni kutokana na mabomu ya kutoa machozi ,” alisema.

Tukei, hata hivyo amesema, wanafunzi 30 kutoka shule hizo mbili za sekondari wamekamatwa kw akuchochea ghasia.

“Naweza kuthibitisha kuwa wanafunzi 30 wametiwa nguvuni kwa kuchochea ghasia na watashtakiwa ipasavyo ,” amesema bwana Tukei.

Washukiwa kwa sasa wanashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi mjini Mbale.

Amesema kuwa wameanza uchunguzi kubaini chanzo cha mapigano hayo.

Bwana Stephen Wambalo, mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Mbale High School, amesema kuwa wananzi waliolazwa, walivuta hewa ya mabomuj ya kutoa machozi, ambayo iliwafanya waapoteze fahamu kabla ya kuanguka.

“Polisi walipoingilia kati kuzima ghasia, walifyatua gesi ya kutoa machozi ambayo iliwafanya wanafunzi wapige mayowe kuomba usaidizi kwani walikuwa wanapungukiwa na hewa safi ya kupumua ” amesema mwalimu Wambalo.

vyanzo: The monitor /bbc

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.