Manchester United huenda ikalazimika kulipa Leicester City £80m kumnunua mlinzi wake Harry Maguire baada ya Eric Bailly kuumia goti katika mechi ya kirafiki dhidi ya Tottenham. (Mirror)

Winga wa Leicester Muingereza Demarai Gray 23- amesema hakuna haja ya kuwa na “hofu” kuhusu uhamisho wa Maguire na kuongeza kuwa haamini nyota huyo wa miaka, 26, ana msongo wa mawazo kuhusu hatma yake. (Leicester Mercury)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amepuuzilia mbali madai kuwa wanamlenga mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 30, na kusisitiza kuwa kipaumbele chake kwa sasa ni kuimarisha kikosi kilichopo badala ya kununua wachezaji wapya. (Independent)

Gareth Bale
Image captionGareth Bale alijiunga na Real Madrid mwaka 2013

Everton imeifahamisha Crystal Palace kuwa wanaandaa dao la £60m kumnunua mshambuliiaji wa Uturuki Cenk Tosun kama sehemu ya mkataba wa kumzuilia mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26 -lakini wanahofia huenda akanyakuliwa na Chelsea. (Telegraph)

Manchester United inajiandaa kumnunua mchezaji wa Lazio na nyota wa kimataifa wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic kare kwa kima cha £70m ,kuchukua nafasi ya kiungo wakati mfaransa Paul Pogba endapo ataamua kuhama klabu hiyo. (Mirror)

Ole Gunnar Solskjaer (left) and Paul Pogba
Image captionOle Gunnar Solskjaer (kushoto) na Paul Pogba

Hata hivyo Kuna tetesi huenda, Pogba akasalia Old Trafford kwa mwaka mwingine mmoja, hatua ambayo huenda ikamnyima nafasi Milinkovic-Savic (Express)

Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo, 34, hana uwezo wa kumshawishi Neymar kujiunga na miamba wa Italia- kwa sababu nyota huyo wa Brazil wa miaka 27-ameamua kujiunga na Barcelona. (Star)

Cristiano Ronaldo
Image captionCristiano Ronaldo

Borussia Dortmund wanafanya mazungumzo ya kumsajili mshambulizi wa Barcelona Malcom kwa euro milioni 42 (£37.5m). (Goal)

Mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Moussa Dembele , 23, atakuwa katika urodha ya kujiunga na Manchester United klabu hiyo ikiamua kumuuza nyota wa kimataifa wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26. (Sky Sports)

Thamani ya uhamisho wa mlinzi wa Spurs Toby Alderweireld imeongezeka mara dufu baada ya masharti ya mkataba wa £25m wa kumuachilia kiungo huyo raia wa Ubelgiji wa miaka 30 kufikia kikomo siku ya Alhamisi. (Sun)

Toby Alderweireld
Image captionMlinzi wa Spurs Toby Alderweireld

Meneja wa Napoli Carlo Ancelotti ana matumaini klabu yake itamsajili mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, 28, kutoka Real Madrid msimu huu. (Marca)

Manchester United huenda wakalazimika kutumia zaidi ya £30m kumpata kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff,21. (Manchester Evening News)

Tottenham imewasiliana na Juventus kuhusu usajili wa nyota wa kimataifa wa Argentina international mshambuliaji Paulo Dybala, 25, ambaye bei yake anayekadiriwa kuwa £80m. (Evening Standard)

Paolo Dybala
Image captionPaolo Dybala

Aston Villa wanakaribia kukamilisha usajili wa mchezaji wa 11 kabla ya dirisha la uhamisho wa wachezaji kufungwa -tayari wametumia £120m – na wanatarajiwa kuilipa klabu ya Brugge £11 ili kumunua mchezaji wa kimataifa wa Zimbabwe Marvelous Nakamba, 25. (Telegraph)

Tetesi Bora Alhamisi

Philippe Coutinho

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amefutilia mbali uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona, Philippe Coutinho, 27, ambaye aliondoka Anfield kwa kima cha £142m mwaka 2018. (ESPN)

Manchester United wameomba kufahamishwa kuhusu hatma ya mchezaji Christian Eriksen, 27, wa Tottenham. Kandarasi ya nyota huyo wa kimataifa wa Denmark amesalia na mwaka mmoja kukamilika na huenda akauzwa kwa pauni milioni 70. (Mail)

Christian Eriksen
Image captionChristian Eriksen

United pia inamlenga mshambuliaji wa Lille na nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Nicolas Pepe, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £70m, kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku endapo atajiunga na Inter Milan. (Times)

Paris St-Germain imekubali kulipa £28m kumsajili kiungo wa kimataifa wa Senegal Idrissa Gueye, 29, kutoka Everton. (Mail)

chanzo: bbc

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.