Mwanamuziki wa Rap na milionea wa Marekani ni amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni miongoni mwa Wanyarwanda, wakidai ana asili ya Rwanda.

Ikiwa Beyoncé aliamua tu kunogesha wimbo wake kwa kutumia maneno hayo, au ni kweli mwanamuziki huyo maarufu wa Marekani ana asili ya Rwanda, mambo haya kuwa ya kawaida kwenye mitandao ya kijamii nchini Rwanda.

Beyoncé Giselle Knowles Charter
Image captionBeyoncé Giselle Knowles Charter

Gumzo hilo la mtandaoni lilitokana na wimbo wa mke wake Jay -Z, Beyoncé Giselle Knowles- Charter aliouita ”Mood 4 Eva” katika albamu yake mpya aliyoiita “The Lion King: The Gift”, ambapo ilisikika akisema: “baby father” has a bloodline- akimaanisha baba wa mtoto wake ana asili ya Rwanda katika wimbo wake.

Katika maandishi ya mistari ya wimbo huo mstari ulioandikwa na kuimbwa kwa maneneo ya lugha ya kiingereza My baby father, bloodline Rwandandio yaliyokonga mioyo ya Wanyarwanda kwenye mitandao ya kijamii:

  • “I’m so unbothered, I’m so unbothered
  • Y’all be so pressed while I’m raisin’ daughters
  • Sons of empires, y’all make me chuckle
  • Stay in your struggle, crystal blue water
  • Piña colada-in’, you stay Ramada Inn
  • My baby father, bloodline Rwanda
  • Why would you try me? Why would you bother?
  • I am Beyoncé Giselle Knowles-Carter” reads a verse from the song, in which she features her husband Jay Z and Childish Gambino.

Wengi wamekuwa wakijaribu kuwaza kuhusu uwezekano wa Jay Z kuwa Myararwanda. Huku baadhi wakidiriki hata kusema kuwa wana undugu wa damu na bilionea huyo.

Baadhi kama Blu, waliujaribu hata kumkejeli Jay-Z akimuamrisha ale mboga ya majani inayoliwa Rwanda:

Baadhi walipeleka mbali gumzo hilo hata kudai kuwa waliwapoteza ndugu au jamaa wanafanana kama bilionea huyo wa muziki wa Rap, huku picha za mizaha zinazomuonyesha Jay Z kama Rwanda zikitumwa kwenye mitandao hiyo.

Jarida linalochapishwa nchini Twanda la The Newtimes limetaja picha moja ya kitambulishi cha taifa iliyofanyiwa uhariri ikionyesha picha ya Jay-Z akiwa na jina linaloaminiwa kuwa ni la Kinyarwanda “Jacques Zirasunda” kwa kifupi likimaanisha kile kilichotajwa kuwa ni JAY Z.

Katika ujumbe mwingine , Wanyarwanda walielezea kwa mzaha jinsi ambavyo Jay Z angekuwa anaishi na mienendo yake kama angelikuwa kweli ni Mnyarwanda.

Huku Jay Z au Beyoncé bado hawajatoa maelezo ya kina juu ya hadidhi ya asili ya yao , Wanyarwanda wengi kwenye mitandao ya kijamii wamemeamua kumfanya ‘Myarwanda’ mwanamuziki huyo wa muziki wa rap nchini Marekani , ambaye anamafanikio makubwa na ambaye amekadiriwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 1 za kimarekani.

Kwa upande mwingine Jean-Baptiste Micomyiza alidai Jay -Z afichue wazi msururu wa kizazi chake ili kuweza kufahamu ni wapi kuna mizizi ya mababu zake nchini Rwanda. GraceIshimwe kwenye ukurasa wa Twitter aliamua kumpataia jina la Kinyarwanda:

katika nyimbo 27 zilizomo katika Albamu , baadhi aliimba mwenyewe huku nyingine akishirikiana na wanamuziki wa Afrika magharibi

Miongoni mwa wanamuziki hao ni ; Tekno, Yemi Alade, Mr Eazi, Tiwa Savage wa Nigeria, John Kani wa Afrika Kusini na Salatiel wa Cameroun.

katika wimbo “Mood 4 Eva” amezungumzia watu na mambo mbali mbali kuhusu bara la Afrikakama vile Nelson Mandela, Jukua Jay-Z akijifananisha na Mansa Musa (Mfalme wa Mali ambaye inasemekana kuwa alikuwa ni mtu wa watu kuliko watu wote duniani).

katika wimbo huu pia Beyoncé anasema yeyeni “Malkia wa Sheba” (Queen of Sheba), ambaye katika historia anasemekana kuondoka Afrika na kwenda kumtembelea mfalme Solomon wa Israeli

katika Albamu hii mpya pia ya Beyoncé aliyoiita ‘Spirit’ inaanza kw amaneneo ya Kiswahili yanayosema ‘Uishi kwa muda mrefu mfalme’

Wanaofuatilia kwa karibu muziki wa Beyoncé na mumewe Jay Z wanasema nyota hawa wanataka kuwakaribia zaidi wapenzi na mashabiki wa muziki wao katika soko jipya la Afrika linalokua kwa kasi.

chanzo:bbc

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.