Watu saba ambao ni wavuvi wamenusuruka kufa baada ya ngalawa yao kuzama maeneo ya kisiwa cha chumbe walipokuwa wakiendelea na shughuli zao za uvuvi.


Kamanda Moh’d Ali wa KMKM amesema wakati walipokuwa wanaendelea na doria zao za kawaida ndipo walikishuhudia chombo ambacho kimepakia wavuvi hao kinazama na ndipo walipoenda kuwaokoa na kufanikiwa kuwapata wote wakiwa salama.

Upepo mkali uliotokea majuzi tarehe tarehe 22/07/019 uliwakumba pia wavuvi saba wa Tumbe wilaya ya Micheweni Pemba

Wavuvi hao walienda kujitafutia riziki wakiwa na ngalawa moja pamoja na mashua na kukumbana na dharuba kubwa ya upepo uliopelekea kushindwa kuendelea na safari ya kurejea majumbani kwao

Vyombo vyao hivyo vilizama mkondoni ambapo baada ya muda kupita ndio walitokezea wavuvi wenzao wa kijiji jirani cha Shumba Mjini na kuweza kuwaokoa na kuwapeleka juu wote wakiwa salama kiroho huku wakiwa wamepoteza vifaa vyote pamoja na ngalawa na mashua

Wavuvi hao ni kama ifuatavyo:-

Ngarawa

1.SEIF BUPU NAHOZA
2.ALI KOMBO KHAMIS
3 ALI JUMA HAMAD
4.KOMBO JUMA KITOMI

MASHUA
1.SALIM KHAMIS MJAJA NAHOZA
2.ABDALLA ISSA ABDALLA
3.HAMAD ALI HASSAN

vyanzo: hassan khamis/wzanzibar24

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.