Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Kwa mara ya kwanza anasafiri kwa treni ya Shirika la TAZARA, kuelekea Rufiji.

Aliingia kwenye moja ya mabehewa ya treni ya TAZARA kwa ajili ya safari ya kuelekea kuweka jiwe la msingi kwenye mradi mkubwa wa kufua umeme katika mto rufiji utakaozalisha umeme wa kilowati 2115

Watu mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti kuhusu hatua ya rais Magufuli kusafiri kwa Treni badala ya usafiri ambao kwa maoni yao wanaona kuwa unamfaa zaidi kwa hadhi yake, wengine wakiona ni jambo jema na kuwataka viongozi wengine ambao hutumia usafiri wa hadhi ya juu kufuata mfano wa rais Magufuli.

Kabla ya kupanda treni, Rais Magufuli amezungumza na viongozi wa TAZARA na kuwataka kuwasilisha mapendekezo yao juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa kuboresha usafirishaji wa mizigo na abiria kupitia TAZARA.Rais Magufuli amesema Serikali inatambua umuhimu wa shirika hilo.

January Makamba afutwa uwaziri Tanzania

Museveni awasili Chato kumtembelea Magufuli

Akizungumza kuhusu changamoto za wafanyakazi rais Magufuli ameutaka uongozi wa shirika hilo kutatua kero za wafanyakazi wa TAZARA kwa mazungumzo ya pande zote mbili.

”Hakikisheni wafanyakazi mnawasaidia hawa wafanyakazi wako frustrated,nimewauliza maswali hawakutaka kuzungumza kwa sababu wameogopa, hawataki kuongea chochote.Si kwamba hawana shida,wana shida kibao, ila wanawaogopa ninyi inawezekana mnawatishia kwamba mtu akizungumza anafukuzwa. Mkae na wafanyakazi mzungumze shida zao mzitatue, zile zinazoshindikana mzilete serikalini”. Alisema Magufuli.Ruka ujumbe wa Twitter wa @dekamu6

dekamu@dekamu6Replying to @MsigwaGerson

Mwamba akikagua miundombinu..tayari kwa safarii11:02 AM – Jul 25, 2019Twitter Ads info and privacySee dekamu’s other Tweets

Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @dekamu6Ruka ujumbe wa Twitter wa @EzekielChengul2

Ezz Chezz@EzekielChengul2Replying to @MsigwaGerson

Tazara is a sleeping giant, a sleeping lion. Something needs to be done. A very great potential left idle. The good thing about Tazara is that it doesn’t need much rebuild. It’s about strategic planning and commitment. The best thing is “he didn’t board that train accidentally”.612:15 AM – Jul 25, 2019Twitter Ads info and privacySee Ezz Chezz’s other Tweets

Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @EzekielChengul2Ruka ujumbe wa Twitter wa @EngUlomi

Eng.Elisante Ulomi@EngUlomiReplying to @MsigwaGerson

Haya ndio mambo anatakiwa kuelezwa mkuu wa nchi,Mambo ya maendeleo nini kifanyike nchi iende mbeleeee.JPM endelea kuchapa kazi.3:08 AM – Jul 25, 2019Twitter Ads info and privacySee Eng.Elisante Ulomi’s other Tweets

Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @EngUlomi

Reli ya Tazara yenye urefu wa kilomita 1,860 ina uwezo wa kusafirisha tani milioni tano za mizigo kwa mwaka, lakini kutokana na upungufu wa injini na mabehewa ya kutosha, inasafirisha chini ya tani 300,000 kwa mwaka.

Reli hiyo ilijengwa kwa msaada kutoka China, ilianza huduma mwaka 1975 na inamilikiwa kwa ubia wa asilimia 50 kwa 50 wa nchi ya Tanzania na Zambia

chanzo:bbc

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.