Jordan imezindua makavazi yake ya kwanza ya kijeshi chini ya bahari katika pwani ya Aqaba.

Katika hafla ya uzinduzi huo siku ya Jumatano, ufalme huo ulizamisha magari kadhaa ya kivita pamoja na helikopta kijeshi chi ya bahari.

Magari hayo yaliegeshwa kana kwamba yako vitani yamewekwa katika miamba ya matumbawe yaliopo chini ya bahari nyekundu.

Mamlaka zinasema onyesho hilo ni mbiniu mpya ya utalii kwa wageni wanaozuru taifa hilo.

Miamba ya matumbawe katika sehemu ya Kaskazini mwa Bahari nyekundu ni kivutio kikubwa kwa wapiga mbizi na watalii wengine

Halmashauri ya eneo maalum la kiuchumi la Aqaba (ASEZA) imeongeza kuwa itajumuisha aina tofauti ya michezo katika “mazingira hayo ya maonesho”.

Helikopta ya kijeshi, iliyotolewa na kikosi cha jeshi la hewa la Jordan, ilikuwa moja ya vyon=mbo vya kijeshi vilivyozamishwa chini ya bahari
Image captionHelikopta ya kijeshi, iliyotolewa na kikosi cha jeshi la hewa la Jordan, ilikuwa moja ya vyon=mbo vya kijeshi vilivyozamishwa chini ya bahari
Halmashauri ya eneo maalum la kiuchumi ya Aqaba imeiambia Jordan Times kuwa ma vifaa hatari vilitolewa ndani ya magari hayo kabla yazamishwe
Image captionHalmashauri ya eneo maalum la kiuchumi ya Aqaba imeiambia Jordan Times kuwa ma vifaa hatari vilitolewa ndani ya magari hayo kabla yazamishwe
Jordanian Armed Forces' armoured vehicle lies on the seabed of the Red Sea off the coast of the southern port city of Aqaba
Image captionWatakaoweza kuzuriu makavazi hayo ni wapiga mbizi wanaotumia vifaa maalum na wataliii wanaotumia maboti maalum yalio na sakafu ya kio
Wapiga mbizi wakitoka ndani ya maji baada ya kuzamisha magari ya kijeshi chini ya bahari nyekundu katika pwani ya Aqaba
Image captionWapiga mbizi wakitoka ndani ya maji baada ya kuzamisha magari ya kijeshi chini ya bahari nyekundu katika pwani ya Aqaba

Picha zotye zina haki miliki.

chanzo:bbc

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.