Data za sensa kuhusu uhamiaji nchini India zinaonyesha kuwa kiwango cha watu kutoka Uganda wanaohamia nchini humo kimeongezeka kwa haraka , kwa kiwango cha maelfu ya watu. Ameelezea mtaalamu wa uhamiaji Chinmay Tumbe anaeleza ni kwanini hii inaweza kuwa ni matokeo kufeli kwa maafisa

India imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Uganda.

Mnamo miaka ya 1890, takriban wahindi 40,000 I wengi wao kutoka Punjabi , waliletwa Uganda kama wafanyakazi wahamiaji kujenga leri ya Uganda inayounganisha nchi hiyo na mji wa Mombasa nchini Kenya hadi Kampala Uganda.

Walilazimishwa kuondoka nchini humo mnamo mwaka 1972 kwa amri ya mtawala wa kijeshi Idi Amin, ambaye aliwashutumu “kunyonya pesa za Uganda”. (wengi wao walirejea tena Uganda miaka ya 1980 na 1990, na kuwa mhimili wa uchumi wa taifa )

Mambo haya yote yalichezwa katika maigizo ya Hollywood kama The Ghost na the Darkness (1996) na The Last King of Scotland (2006).

Sasa, katika mwaka 2019, uhusiano watatu umeanzishwa kati ya India na Uganda – na mara hii ni wa kiwango cha juu, umetoka katika sensa ya kuanzia mwaka 2011 ya India. Kazi hiyo ya kuhesabu idadi ya watu hufanyika kila baada ya miaka 10, lakini baadhi ya data zijnatolewa sasa.

Idadi ya watu nchini India imeongezeka kutoka kiwango cha watu milioni 181 hadi bilioni 1.21 kwa kipindi cha muongo mmoja tangu 2011, kwamujibu wa matokeo ya sensa.

Wahindi waliokuwa wakiishi nchini Uganda walilazimika kuondoka mnamo mwaka 1972
Image captionWahindi waliokuwa wakiishi nchini Uganda walilazimika kuondoka mnamo mwaka 1972

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni na idara ya uhamiaji , Idadi ya Wahindi walioripoti kuwa Uganda ndio eneo lao la mwisho la makazi iliongezeka kutoka watu 694 mwaka 2001 hadi watu 151,363 mwaka 2011.

Ongezeko hili lilidhihirika zaidi miongoni mwa wanawake ambao waliongezeka kutoka – 339 hadi 111,700 – kuliko wanaume ambao walikuwa ni 355 na kufikia 39,663.

Baada ya mataifa ya kikanda ya Bangladesh, Nepal, Pakistan na Sri Lanka, sasa ni Uganda katika Afrika ambayo inaonekana kuwa chanzo cha uhamiaji wa hali ya juu au kurejea kwa uhamiaji nchini India. Hii inaweza kudhihirishwa na Waganda ambao wamehamia India au Wahindi wanaoishi Uganda na ambao wamerudi.

Kinyume na karne iliyopita, Uhusiano na Punjabi ni mdogo. Katika jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh na jimbo la mashariki la Bihar,idadi ya wahamiaji Waganda au wahamiaji waliorejea imepanda kutoka watano mwaka 2001 hadi 94,704 mwaka 2011.

Idadi hii inaonyesha mambo mawili.

Kwanza , ni kielelezo rahisi juu ya ongezeko la kutokuwepo kwa uwiano wa idadi ya jinsia za kike na kiume.

Pia zaidi ya 77,000 ya Wahamiaji hawa wa Uganda au wanaporejea waliripoti kuwa wamekuwa nchini India kwa zaidi ya miaka kumi . Lakini sensa ya mwaka 2001 iliwahesabu jumla ya waganda wa aina hiyo 694.

Idadi ya watu wa ndia itapanda na kufikia kati ya 1.6 na 1.8 billioni ifikapo mwaka 2060
Image captionIdadi ya watu wa ndia itapanda na kufikia kati ya 1.6 na 1.8 billioni ifikapo mwaka 2060

Swali la sensa limewekwa katika waraka mfupi na wanaohesabiwa wanatakiwa kuandika jina la nchi kwenye karatasi ikiwa watu walifika kwenye makazi yao ya mwisho wanapokuwa nje ya India.

Karatasi hizi baadae huchunguzwa na software ya kompyuta ambayo hutengeneza jedwali. Karatasi hizi hatimae hupakuliwa kwenye tovuti na kutangazwa kwa umma.

Afisa wa ngazi ya juu wa sensa ameiambia BBC kuwa ofisi yake inachunguza “uwezekano wa idadi ya wahamiaji ambao huenda Uganda haikuwa makazi yao ya mwisho”

chanzo:bbc

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.