Kiongozi aliyechaguliwa kwa huru rais Beji Caid Essebsi amefariki akiwa na miaka 92, ikulu ya nchi hiyo imeeleza.

Alikuwa kiongozi mkongwe zaidi duniani. Alilazwa hospitali Jumatano lakini maafisa hawakueleza kwanini alipelekwa kupokea matibabu.

Essebsi alishinda uchaguzi huru wa kwanza Tunisia mnamo 2014 kufuatia vuguvugu la maandamano katika mataifa ya kiarabu.

Alilazwa hospitalini mwezi uliopita baada ya kukabiliwa na maafisa wanachotaja kuwa hali mbaya ya afya.

Hawakutoa ufafanuzi zaidi wakati huo.

Waziri mkuu Youssef Chahed, aliyemtembelea hospitalini, aliwaomba watu kuacha kusambaa habari za uongo kuhusu hali yake.

Mapema mwaka huu, Essebsi alitangaza kwamba hatogombea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa Novemba.

Aliwaambia wajumbe wa chama chake tawala Nidaa Tounes katika mkutano kwamba kijana anahitajika kuchukua uongozi. Alisema muda umewadia “kuwafungulia mlango vijana”.

Aliyekuwa rais wa Tunisia Zine el-Abedine Ben Ali alitimuliwa madarakani mnamo 2011 baada ya kuhudumu kwa miaka 23 madarakani.

Tangu hapo , Tunisia imeshinda sifa kama taifa la pekee lililoibuka kutoka mapinduzi na kuingia katika demokrasia baad aya vuguvugu katika nchi za kiarabu.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni, taifa hilo limekabiliwa na mashambulio utoka kwa wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu na matatizo ya kiuchumi, huku ukosefu wa ajira ukikithiri.

chanzo:bbc

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.