Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amepiga marufuku mtu yeyote kuimba wimbo wa taifa bila uwepo wake, amesema waziri wa habari Michael Makuei ambaye pia ni msemaji wa serikali.

Bw. Makuei amesema ameliambia shirika la Habari la AFP kuwa viongoz tofauti na wa ku wa taasisi za umma wamekuwa wakiimbiwa wimbo wa taifa bila sababu zozozte za msingi na kuongeza kuwa hatua hiyo ni ya kutumia vuibaya wimbo huo ambao ulitungwa muda mfupi baada ya taifa hilo kupata uhuru wake mwaka 2011.

“Kwa taarifa ya kila mmoja wimbo wa taifa ni wa Rais peke yake, na utaibwa tu katika hafla inayohudhuriwa na rais , sio ya kila mtu,” Makuei alisema.

“Tumeshuhudia waimbo wa taifa ukipigwa katika hafla zinazohudhuriwa na waziri, makatibu wakuu na hata magavana wa majimbo.”

Ameongeza kuwa amri hiyo imetolewa na rais wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri siku chache zilizopita.

Makuei pia amefafanua kuwa wimbo wa taifa utapigwa katika ubalozi ya Sudan Kusini nje ya nchi kwa niaba ya rais na shuleni ambako watoto wanafunzwa kuimba wimbo huo bila uwepo wa Bw. Kiir.Ruka ujumbe wa Twitter wa @JubaDailyNews

Juba Daily News@JubaDailyNews

Sing #SouthSudan national anthem on your own risk citizens warned, directives issued by SouthSudan embattled Pres. Kirr has banned singing of nation anthem. “These are orders and of course when you disobey the orders of the president then you carry your cross,” Michael Makuei

View image on Twitter

2:49 PM – Jul 22, 2019Twitter Ads info and privacySee Juba Daily News’s other Tweets

Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @JubaDailyNews

Haijabainika ni adhabu gani itatolewa kwa yeyote atakaye kiuka amri hiyo ya rais.

“Hii ni amri ya rais na bila shaka ukiivunja utabeba msalaba wako mwenyewe,” Makuei alisema.

Haijabainika kwa nini Kiir ameamua kuubinafsisha wimbo wa taifa kwasababu wimbo huo ni nembo ya taifa inayowaleta watu pamoja.

Amri nyingine iliyotolewa na rais Kiir, inalenga viongozi wa kijeshi ambao sasa wamepigwa marufuku kuhutubia mukutano wa hadhara wakiwa wamevalia sare zao za kazi.

Sudan Kusini ilipata uhuru wake mwaka 2011 baada ya kujitenga na Sudankufuatia kura ya maoni na Bw Kiir amekuwa akiliongoza taifa hilo tangu wakati huo.

Hatua ya hii inajiri waka ambapo rais huyo amekubali kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na kiongozi wa upinzani Riek Machar, katika kile kinachoonikana kuwa hatua ya kufufua upya mazungumzo ya amani ambayo yalikwama na kusababisha vurugu katika taifa hilo.

Katika barua iliyowasilishwa hivi karibuni na mshauri wa rais, Tut Gatluak, Bw Machar amesema yuko tayari kukutana na ra alimradi atakuwa huru kuzuru Sudan Kusini.

Utawala wa Bwana Kiir umemualika Machar baada ya serikali na makundi ya upinzani kushindwa kufikia muda wa mwisho wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ambao ulikuwa mwezi Mei.

Muda huo sasa umesongezwa mbele kwa miezi sita zaidi.

chanzo:bbc

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.