Uchunguzi mpya umetoa mwangaza juu ya jinsi baadhi ya nchi maskini zaidi za Afrika zinavyopoteza mamilioni ya dola za mapato ya kodi kutoka makampuni ya kimataifa na matajiri binafsi.

Ripoti kutoka Muungano wa kimataifa wa waandishi wa habari wa taarifa za uchunguzi -International Consortium of Investigative Journalists, inasema kuwa makampuni na watu binafsi hutumia taifa la kisiwa lililopo kwenye bahari ya Hindi la Mauritius kuepuka kisheria kulipa kodi kubwa, katika nchi ambazo wanafanyia biashara zao.

Mauritius inakanusha kufanya kosa lolote na inasema inatekeleza sheria husika za kimataifa.

Ripoti hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia nyaraka 200,000 za siri ambazo zinaonyesha kwa mara ya kwanza ni kwa jinsi gani makampuni ya sheria ya kigeni yalivyosaidia wateja wake wa kigeni kuepuka kulipa mamilioni ya dola ya kodi.

Kisiwa cha Mauritius kimekuwa kikitumiwa na makampuni na watu binafsi kutoka mataifa maskini zaidi kukwepa kulipa kodi za mapato
Image captionKisiwa cha Mauritius kimekuwa kikitumiwa na makampuni na watu binafsi kutoka mataifa maskini zaidi kukwepa kulipa kodi za mapato

Taarifa za rekodi za siri, barua pepe na mafaili, zilizoitwa ufichuzi wa Mauritius, zinafichua utendaji wa kisheria ambao unasaidia kukwepa mapato ya kodi unaofanywa na watu kutoka mataifa ya Afrika , Mashariki ya kati na Asia na kupelekwa mifukoni mwa makampuni ya magharibi , huku Mauritius ikipata sehemu yake.

Nyaraka hizo zimetoka katika ofisi ya Mauritius ya kampuni ya sheria yenye makao yake Bermuda inayofahamika kama -Conyers, Dill & Pearman, na nyaraka hizo zinaonyesha taarifa za kipindi cha kuanzia miaka ya 1990 hadi 2017.

BBC bado haijachunguza ripoti hii kuthibitisha ukweli kuihusu.

Nyaraka hizo zinajumuisha taarifa za akaunti za benki ambazo zinayahusisha makampuni ya kimataifa na makampuni ya uhasibu katika usafirishaji wa pesa wenye utata unaolenga kuepuka malipo ya kodi.

Ramani inayoonyesha lilipo taifa la Mauritius
Image captionRamani inayoonyesha lilipo taifa la Mauritius

Uchunguzi huo unasema kuwa makampuni yalitumia mikataba 46 ya kosi ambayo Mauritius inayo na mataifa maskini zaidi duniani, ukosefu wa mapato ya mtaji na sheria dhaifu, kusajili makampuni ya mafuta ya shell katika taifa hilo lililopo kisiwani ingawa hawakuwa na wafanyakazi au shughuli zao huko.

Kampuni ya sheria Conyers iliuza ofisi yake ya Mauritius kwa wafanyakazi wake wa zamani mnamo mwaka 2017 na kusema kuwa inadhibitiwa na sheria katika nchi ambako zinafanyia kazi.

Mauritius imeimarisha sheria zake juu ya makampuni ya kigeni, lakini baadhi ya wataalamu wa masuala ya kodi bado wanaona ni njia ya uongo inayoruhusu uepukaji na ukwepaji wa kodi.

chanzo:bbc

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.