Israel imeanza kubomoa makaazi kadhaa ya wapalestina ambayo inasema yalijengwa kinyume cha sheria karibu sana na eneo linalougawanya ukingo wa magharibi.

Maafisa wa usalama wameinga katika eneo la Sur Baher, katika eneo la Jerusalem mashariki, kuzibomoa nyumba hizo zinazoarifiwa kuwahifadhi watu 17.

Wakaazi wanasema walipewa vibali vya kuwaruhusu kujenga na mamlaka ya Palestina, na wameishutumu Israel kwa kujaribu kuinyakua ardhihiyo ya ukingo wa magharibi.

Lakini mahakama ya juu zaidi ya Israel iliamua kwamba walikiuka marufuku ya kutojenga katika eneo hilo.

Israel ililidhibiti eneo hilo la ukingo wa magharibi mnamo 1967 katika vita vya mashariki ya kati na baadaye kulitenga eneo la Jerusalem mashariki.Kwa mujibu wa sheria za kimataifa maeneo yote yanatazamwa kuwa makaazi yaliokaliwa, licha ya kwamba Israel inalipinga hilo.

Palestinians watch Israeli army excavator demolishing a building in Wadi Hummus, in the occupied West Bank (22 July 2019)
Image captionWakaazi wanasema walipewa vibali vya kuwaruhusu kujenga na mamlaka ya Palestina

Kiasi ya maafisa 700 wa polisi wa Israeli na wanajeshi 200 walihusiaka katika operesheni hiyo leo katika kijiji cha Wadi Hummus, ukingoni mwa Sur Baher.

Waliingia wakiwa wamejihami kwa matinga matinga yalioanza kubomoa majengo hayo 10 ambayo Umoja wa mataifa ulisema yalikuwa yamelengwa kubomolewa.

Raia tisa wa Palestina walioathirika ni wakimbizi wakiwemo watoto watani kwa mujibu wa Umoja wa mataifa. Wengine 350 waliokuwana makaazi katika eneo hilo lakini ambayo hayana watu au yalikuwa bado yanajengwa pia wameathirika.

Mmoja wa wakaazi hao, Ismail Abadiyeh, ameliambia shirika la AFP kuwa familia yake ‘itasalia barabarani’.Hakimiliki ya Picha @nadplo@NADPLO

Waziri mkuu katika mamlaka ya Palestina Mohammad Shtayyeh amesema raia wa Palestina watalalamika katika mahakama ya kimataifa ya jinai ICC kuhusu ‘uchokozi huo mkubwa’.

“Huu ni muendelezo wa kuwatoa watu kwa lazima katika makaazi yao na ardhi zao – uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu,” ameongeza

Lakini waziri wa usalama wa umma Gilad Erdan amesema mahakamaya juu zaidi ya Israel ” iliamua pasi na shka kwamba majengo hayo yalijengwa kinyume cha sheria karibu na ua wa usalama na kutishia maisha ya raia na vikosi vya usalama”.

Mratibu wa misaada ya kibinaadamu katika Umoja wa mataifa Jamie McGoldrick aliiomba Israel wiki iliyopita kufutilia mbali ubomoaji huo na badala yake iidhinishe “sera za usawa za upangaji” kwa wapalestina.

Israel pulls down a cluster of Palestinian homes

Ubomoaji katika eneo hilo la Wadi Hummus kwa kawaida hukumbwa na mzozo kwasababu majengo yaliopo katika sehemu za ukingo wa magharibi chini ya mamlaka ya Palestina lakini yalio katika upande wa Israeli linaloyagawanya maeneo hayo.

Vizuizi hivyo vilijenga ndani na katika maenoe yanayopakana na ukingo wa magharibi kufuatia vuguvu au intifada ya pili ya Palestina lililoanza mnamo 2000.

Israel inasema lengo la kizuizi hichi ni kuzuia washambuliaji wa Palestina kupenya kutoka ukingo wa magharibi, lakini Palestina inasema ni chombo cha kunyakua ardhi iliyokaliwa.

chanzo: bbc

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.