Wapalestina wanaadhimisha miaka 71 ya kuachwa bila makao wakati wa vita vya 1948 vilivyopelekea kubuniwa kwa taifa la Israel.

Maandamano yamefanyika kote katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza leo kuadhimisha kile ambacho Wapalestina wanakiita “Nakba” au “maangamizi.”
Kumezuka machafuko pia baina ya waandamanaji hao na wanajeshi wa Israel katika uzio wa waya ulioko Ukingo wa Magharibi na Israel.
Mamia ya maelfu ya Wapalestina walikimbia au walifukuzwa kwa lazima kutoka makaazi yao wakati wa vita hivyo.
Leo hii inakadiriwa kuwa kuna karibu Wapalestina milioni tano ambao ni wakimbizi kote Mashariki ya Kati.
Katika mji wa Ukingo wa Magharibi wa Ramallah mamia ya watu waliandamana kutoka kwenye kaburi la kiongozi wa zamani wa Palestina, Yasser Arafat, wakitaka haki ya kurudi kwenye ardhi zao katika eneo ambalo sasa ni Israel.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.