Mmoja wa wakosoaji wakuu wa Rais John Magufuli wa Tanzania, ambaye alishukiwa kutekwa takribani wiki moja iliyopita, amepatikana usiku wa kuamkia leo akiwa amepigwa vibaya na sasa amefikishwa hospitalini, kwa mujibu wa chama kikuu cha upinzani nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na CHADEMA inasema Mdude Nyangali, ambaye pia mfuasi wa chama hicho, alikamatwa na watu wanne waliokuwa na silaha wakati akitoka kazini huko Mbozi, kusini magharibi mwa Tanzania, siku ya Jumamosi.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Vincent Mashinji, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Nyangali amepigwa vibaya sana hawezi kutembea. Alipatikana akiwa ametupwa katika kijiji kimoja kilicho umbali wa kilomita 70 kutoka mahala anapoishi.

Kampeni kubwa ya mtandaoni ilianzishwa mara tu baada ya tukio hilo kuripotiwa, huku wanaharakati, wanasiasa, wanasheria na wananchi kadhaa wakijiunga nayo kutaka kuachiliwa haraka kwa kijana huyo.

Chanzo: DW Swahili

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.