Waziri wa zamani wa nishati na madini wa Tanzania Bara, William Ngeleja, anasema amezirejesha fedha zote alizopewa ‘msaada’ na mfanyabiashara James Rugemalira mwaka 2014, akidai kuwa hakujuwa kuwa fedha hizo zilihusiana na kashfa ya ufisadi wa Akaunti ya Tegeta Escrow.

Katika taarifa yake iliyosambazwa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo, Ngeleja ambaye kwa sasa ni mbunge wa Sengerema, amesema kwamba anazirejesha fedha hizo ili kulinda heshima yake na ya chama chake, baada ya kuwa mtumishi wa ngazi za juu wa umma kwa miaka 12. Zaidi soma tamko lake hapo chini.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.