Mwanamme wa kwanza kuwahi kupata ujauzito nchini Uingereza amejifunguwa salama mtoto wa kike. 

Hayden Cross mwenye umri wa miaka 21 alipata umaarufu duniani pale alipotangaza kwamba ana ujauzito kutokana na mbegu za kiume alizochangiwa, ikiwa ni miaka mitatu baada ya kutambuliwa rasmi kisheria kuwa ni mwanamme. 


Alizuia mchakato wake wa kuwa mwanamme kamili ili kwanza apate mtoto.

Bintiye aliyempa jina la Trinity-Leigh alizaliwa kwa operesheni tarehe 16 Juni, kwa mujibu wa familia yake, na kumfanya Cross kuwa mtu wa kwanza aliyebabilisha maumbile nchini Uingereza kujifunguwa. 

“Binti yangu yuko salama usalimini”, aliliambia gazeti la mambo ya udaku nchini humo, The Sun. 

Cross, ambaye alizaliwa akiwa mwanamke kwa jina la Page, alikuwa ameomba mayai yake yahifadhiwe kwa matumaini kwamba siku moja angelipata mfadhili wa kumpa mbegu na hivyo kupata watoto. Lakini alipokataliwa, alikutana na mfadhili kwenye kundi moja la Facebook ambaye alikuwa tayari kumpa mbegu yake, na hivyo akaamuwa kuzuia kwa muda mchakato wa kuelekea kuwa mwanamme moja kwa moja ili apate kwanza kubeba ujauzito na kuzaa. 

“Kuwa na mwanangu mwenyewe wa kumzaa daima kumekuwa na maana kubwa kwangu,” alisema mapema mwaka huu. “Daima nilitaka kuwa na watoto.” 

Binti yake alizaliwa kwenye Hospitali ya Kifalme ya Gloucestershire, na kusajiliwa Jumatano iliyopita kwenye Ofisi ya Tarjisi ya Gloucester, ambapo Cross ametajwa kama mama lakini hakuna jina la baba wa mtoto huyo lililowekwa. 

Chanzo: Imetafsiriwa kutoka mtandao wa gazeti la The Independent la Uingereza, 10 Juni 2017. 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.