Mtoto Masoud Khalfan Sanani ana umri wa miaka minane na ni mwanafunzi wa skuli ya msingi. Anaishi na wazazi, bibi na ndugu zake, Fuoni Michenzani, kando kidogo ya kitovu cha mji mkuu wa Zanzibar.

Kwa muda mrefu, Masoud anasumbuliwa na maradhi ya saratani ya damu (leukemia) ambayo bado ingali kwenye hatua yake ya awali na, hivyo, uwezekano wa kutibiwa na kupona kabisa upo, ikiwa atapatiwa matibabu ya haraka.

Hata hivyo, kutokana na hali ya maisha ya nyumbani kwao, wazazi wake hawana uwezo wa kupata shilingi milioni moja na laki mbili za Kitanzania (1,200,000) ambazo zinahitajika kumtibia mtoto wao. Kiwango hicho cha fedha kinaweza kugharamikia sindano za mionzi ambazo anatakiwa kudunga moja kwa kila mwezi ndani ya kipindi cha miezi sita.

Kwa minajili hiyo, Zanzibar Daima inachukuwa nafasi hii kumuombea mchango wako kwake. Tafadhali tuma mchango wako kupitia TIGO PESA nambari +255 713 360 937 ambayo imesajiliwa kwa jina la Salama Hadiy. Unaweza pia kuwasiliana na wazazi wake kwa nambari +255 777 870 004 ili upate maelekezo.

Kutoa ni moyo na ni akiba yako.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.