Taarifa kutoka kisiwani Unguja zinasema kuwa kwa mara nyengine tena kundi la kiharamia, linalofahamika na wakaazi wa kisiwa hicho kama Mazombi, limemvamia, kumpiga na kumuibia kijana mmoja na kumuwacha mahututi.

https://soundcloud.com/mohammed-k-ghassani/mazombi-washambulia-tena

Kwa mujibu wa mama wa kijana huyo, Bi Rukia Ali Faki, mwanawe aitwaje Abdullah Ahmeid Juma (miaka 29), mkaazi wa Mchangani, ni mfanya biashara ndogondogo ya kutembeza mkononi baada ya kuvunjiwa kontena lake hivi karibuni maeneo ya Michenzani.

Mashahidi wanasema Mazombi hao wamemnyang’anya kila kitu, huku wakimvua nguo na kumchoma moto mikononi na miguuni kabla ya kumpora fedha taslim shilingi 800,000 pamoja na kila kitu alichokuwanacho.

 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.