Kundi moja lenye silaha nchini Libya linasema limemuachia huru Saif al-Islam, mtoto wa kiume wa Marehemu Muammar Gaddafi, ambaye alikuwa kizuizini tangu Novemba 2011, kwa mujibu wa gazeti la The Guardian la Uingereza. 

Kundi hilo, Abu Bakr al-Sadiq Brigade linaloundwa na waasi wa zamani na linaudhibiti mji wa Zintan ulio magharibi mwa Libya, linasema Islam aliachiliwa “jioni ya Ijumaa tarehe 14 Ramadhan”, chini ya sherehe ya msamaha iliyopitishwa na bunge lililoko mashariki mwa nchi hiyo iliyosambaratishwa kwa vita tangu kupinduliwa na kuuawa kwaMuammar Gaddafi. 00b;
“Tumeamua kumkomboa Saif al-Islam Muammar Gaddafi. Hivi sasa yuko huru na ameondoka mji wa Zintan,” inasema taarifa ya kundi hilo. 

Zintan inadhibitiwa na makundi yenye silaha ambayo hayakubaliani na serikali ya kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa. 

Islam anatakiwa kukamatwa kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinaadamu unaotajwa kufanyika ndani ya kipindi cha miezi minane wakati wa wimbi la mapinduzi mwaka 2011. 

Hata hivyo, serikali ya Libya na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wanalumbana juu ya nani mwenye haki ya kumhukumu. 

Saif al-Islam, 44, alizaliwa tarehe 25 Juni 1972. Jina lake linamaanisha upanga wa Uislamu na ni mtoto wa pili kati ya wanane wa Gaddafi, akiwa wa kwanza kabisa kati ya watoto wa kiume wa mkewe wa pili, Safiya. 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.