Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM – Tanzania Bara),  Rodrick Mpogolo, akimkabidhi ilani ya uchaguzi ya CCM Mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Mghirwa, mara tu baada ya kuapishwa na Rais John Pombe Magufuli leo asubuhi jijini Dar es Salaam.

Rais John Magufuli alimteuwa Mama Mghwira aliyekuwa mgombea mwenzake wa urais kwenye uchaguzi wa 2015 kupitia chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo kuchukuwa nafasi iliyowachwa na Said Mecky Sadiki, ambaye alijiuzulu nafasi hiyo mwezi uliopita.

Mama Mghwira anakuwa kiongozi wa pili wa chama hicho kinachofuata siasa za mrengo wa kushoto kuteuliwa kuingia kwenye serikali ya Rais Magufuli, akitanguliwa na Profesa Kitila Mkumbo, ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Maji na Umwagiliaji.


Mkuu mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira, akipanga gari lake la ukuu wa mkoa mara baada ya kula kiapo cha kushika wadhifa huo hivi leo.

Hata hivyo, Profesa Mkumbo na Mama Mghwira si wapinzani pekee ambao wameteuliwa kuhudumu kwenye serikali ya Rais Magufuli, kwani walitanguliwa na Augustine Mrema, mwenyekiti wa TLP na pia mgombea urais, ambaye alipewa nafasi ya ukuu wa parole.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.