Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, leo amezinduwa rasmi jengo la ofisi za chama hicho ambazo zitatumika kama ofisi ya wabunge na vile vile kama eneo mbadala kwa shughuli za ofisi kutokana na kile alichokieleza kama kukwepa shari ya inayoitwa ‘kambi ya mwenyekiti anayetambuliwa na msajili’, Profesa Ibrahim Lipumba. 


Aidha kiongozi huyo ameelezea kufikia pazuri kwa madai ya Wazanzibari kuhusiana na uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015 ambapo CUF ilielekea kushinda uchaguzi huo kabla ya kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

“Mambo ni mazuri. Kinachoendelea sasa ni mithili ya ndoana kwenye koo la CCM (Chama cha Mapinduzi). Haki iko karibu kupatikana, ” alisema Maalim Seif katika uzinduzi wa ofisi hizo, ingawa alikataa kuzungumzia undani wa suala hilo kwa madai kwamba ni siri ya watu ambayo hapaswi kuianika hadharani. 

Kupata undani wa tukio zima la leo usikose kutazama Zaima Politiki kupitia ZaimaTV. 

2 thoughts on “CUF yahamia ofisi mpya, yamuachia Lipumba Buguruni”

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.