Rais John Magufuli amemteuwa aliyekuwa mgombea mwenzake wa urais kwenye uchaguzi wa 2015 kupitia chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo kuwa mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro kujaza nafasi iliyowachwa na Said Mecky Sadiki, ambaye alijiuzulu nafasi hiyo mwezi uliopita.

Bi Anna Mghwira anakuwa kiongozi wa pili wa chama hicho kinachofuata siasa za mrengo wa kushoto kuteuliwa kuingia kwenye serikali ya Rais Magufuli, akitanguliwa na Profesa Kitila Mkumbo, ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Maji na Umwagiliaji.

Barua ya uteuzi iliyotolewa muda mfupi uliopita na Ikulu jijini Dar es Salaam inasema pia kuwa Rais Magufuli amewateuwa maafisa wawili wa ngazi za juu kutoka vyombo vya ulinzi na usalama kuwa mabalozi. Maafisa hao ni Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor aliyekuwa mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na DIGP Abdulrahman Omar Juma Kaniki aliyekuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.