Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

 

Hatua hiyo inajiri masaa machache tu tangu Rais Magufuli kumtaka mwenyewe Profesa Muhongo ajiondowe kwenye nafasi hiyo kufuatia kuwasilishwa kwa ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini unaosafirishwa nje inayotilia shaka utendaji wake.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu inasema nafasi hiyo iko wazi na itajazwa baadaye, bila ya kutaja sababu halisi za uamuzi huo.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.