Asubuhi ya leo imeamka na salamu za rambirambi, vilio na majonzi nchini Uingereza, kufuatia vifo vya watu 22 waliouawa kwenye mashambulizi ya kujitoa muhanga usiku katika uwanja wa michezo wa Manchester Arena. 

Mashambulizi hayo yaliyowajeruhi pia watu wengine 59 yanatajwa kufanywa na mshambuliaji aliyejifunga mabomu na kujiripua na kufa pamoja na wahanga hao uwanjani hapo, kwa mujibu wa Idara ya Polisi ya Greater Manchester (GMP). 

Hayo ni mashambulizi mabaya kabisa kuwahi kutokezea ndani ya ardhi ya Uingereza tangu yale ya Julai 7, 2015 ambayo yaliangamiza maisha ya watu 56.

Akizungumza asubuhi ya leo (Mei 23), Mkuu wa Polisi wa GMP, Ian Hopkins, alisema tukio hili “la kuogofya kabisa kuwahi kuukabili” mji huo. 

“Wanafamilia na vijana wengi walikuwa wamekwenda kuburudika na onesho la muziki kwenye Manchester Arena na sasa wamepoteza maisha yao. Tunawalilia marehemu wetu 22 tunaojuwa kuwa wameshatutoka, watu 59 waliojeruhiwa na tunaomboleza pamoja na wapendwa wao. Tunafanya kila tuwezalo kuwasaidia. Majeruhi wanatibiwa kwenye hospitali mbalimbali za Manchester”, amesema Hopkins. 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.