Mbunge wa Mwanakwerekwe, Ali Salim Khamis, leo ametembelea baadhi ya skuli kwenye jimbo lake kushuhudia uhalisia wa mambo ulivyo, ambapo katika moja ya skuli hizo aliungana na wanafunzi kukaa chini kucheza nao.

Wakati dunia ikiwa kwenye karne ya 21, bado ni jambo la kawaida kwa wanafunzi visiwani Zanzibar kukaa sakafuni si kwa kupenda, bali kwa kuwa ndicho walichonacho.

Katika ziara ya leo, Mbunge Ali Salim aliwatembelea pia na kuwafariji waliopatwa na janga la upepo na nyumba zao kuezuliwa. Amechangia bati kwa familia 12.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.