Mwanamme mmoja nchini Uingereza aliyebakiwa na siku chache tu za kuishi amemuowa mchumba wake wa siku nyingi, baada ya sherehe ya harusi iliyoandaliwa masaa 24 tu na wasamaria wema, linaripoti gazeti la Daily Mirror.

Likilinukuu gazeti la Manchester Evening News, Mirror linasema Ray Kershaw, mwenye umri wa miaka 63, na Tracy Brooks, mwenye umri wa miaka 45, walikuwa wametarajia kufunga pingu za maisha mjini Tenerife mwakani, lakini wakajikuta wakiishia na ndoa ya papo kwa papo juzi Jumamosi baada ya Ray kugundulika ana saratani isiyoweza tena kutibika mwezi Machi mwaka huu.

Masaa machache tu baada ya kuchapisha ombi lao mtandaoni, wafanyabiashara na watu wa kawaida kadhaa waliojitokeza kutoa msaada wa kulipia kila kitu kuhusu ndoa yao, kutoka magari ya harusi, mauwa, nguo za kuvaa, keki na kila ambacho kilihitajika kwa sherehe hiyo. 

Ray, ambaye ana saratani ya utumbo mdogo, ana siku chache tu za kuishi na kwa sasa anahudumiwa kwenye kituo cha huduma kwa wagonjwa wa aina hiyo cha Springhill Hospice mjini Rochdale, England. 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.