Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Fredrick Sumaye, ameamua kujiuzulu ujumbe wa Bodi ya Benki ya Maendeleo (CRDB) akisema hataki benki hiyo kupatishwa tabu kwa sababu za misimamo yake ya kisiasa.

Hatua hii inatajwa na wachunguzi wa mambo kuwa ama inaashiria kuwa CRDB imejikuta kwenye wakati mgumu kuwa na mjumbe huyo ambaye aliichachafya vibaya CCM baada ya kujiunga na upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 au alama ya juu ya uwajibikaji na upevu wa kisiasa wa Sumaye binafsi.

Wanasiasa wengi wa ngazi za juu wamo kwenye bodi kadhaa za mashirika ya umma na hawana uthubutu wa kujiondoa.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.