Ripoti kutoka Arusha zinasema kuwa Mstahiki Meya Kalist Lazaro amekamatwa na polisi akiwa kwenye maeneo ya Shule ya Mtakatifu Lucky Vicent, alipokwenda kupeleka mkono wa rambirambi.

Pamoja na meya huyo, amekamatwa pia diwani wa Kata ya Olasiti, Alex Martin, viongozi wa shule hiyo na viongozi wengine wa serikali za mitaa ambao walikuwa wameongozana wa baadhi ya wamiliki wa shule binafsi kuwasilisha rambirambi zao moja kwa moja kwa wenzao waliopatwa na ajali iliyoangamiza maisha ya watu 35 hivi karibuni.

Mashahidi wanasema kuwa kamatakamata hiyo imewajumuisha pia viongozi mbalimbali wa dini, waandishi wa habari na msaidizi maalum wa mbunge Arusha, Innocent Kisanyange.

Inasemekana Meya Lazaro aliamua mwenyewe kuwasilisha fedha za rambirambi moja kwa moja kwa shule hiyo na kwa baadhi ya familia za waliofiliwa na watoto na jamaa zao, badala ya kupitishia serikali ya mkoa inayotuhumiwa kwenye matumizi ya rambirambi za awali.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.