Hadi hivi karibuni, mambo ya urembo na vipodozi yalikuwa mambo ya mtu binafsi. Wanawake wanaojiremba na kujipodoa, walifanya hivyo kwa mafunzo waliyopata kutoka kwa watu wao wa karibu – mabibi, mashangazi, mama, mashoga na au kuiga wayaonayo mitaani. Urembo haukuwahi kuwa sekta rasmi inayojitegemea wala kutambuliwa. Lakini hayo ni ya kale. Sasa urembo ni sanaa na taaluma maalum, yenye wataalamu wake waliobobea na wanaotoa taaluma kama vile ambavyo kuna wanasheria, wahandisi, madaktari na wengineo.

Ndiyo hadithi iliyo nyuma ya Chuo cha Urembo cha Manjano Beauty Academy, kilichopo Barabara ya Shekilango, kando kidogo ya jiji kubwa kabisa la kibiashara la Tanzania, Dar es Salaam. Sheikha Nasser ndiye muanzilishi na mmiliki wa chuo hiki, akiwa pia mkurugenzi mkuu wa Taasisi wa Manjano Foundation.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.