Aliyekuwa naibu waziri wa fedha kwenye serikali ya awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoongozwa na Jakaya Kikwete, Adam Kighoma Ali Malima, amejikuta akikabiliana uso kwa uso na “ghadhabu” za askari wa jeshi la polisi, baada ya kulumbana nao juu ya kile kinachoonekana kama uegeshaji gari mahala pasipostahiki.

Kwenye vidio iliyosambazwa mitandaoni, Malima,  ambaye hivi karibuni pia alikumbwa na zahama ya Chama chake cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma, anaonekana kutupiana maneno na askari wawili waliokuwa nyuma ya gari aina ya Land Cruiser, akiwa na wananchi kadhaa ambao wako upande wake, akiwahoji kwa ukali juu ya hatua wanayochukuwa.

Hata hivyo, hali inabadilika ghafla baada ya mmoja wa askari hao kukoki bunduki yake na kuanza kurusha risasi hewani, ambapo angalau milio mitatu inasikikana kwenye vidio hii hapo chini.

 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.