Jana kwenye mitandao ya kijamii kulisambazwa picha ya maiti ya kijana mwenye ndevu, kofia, kanzu na alama ya sijida usoni ikiwa imelala chini ikichiria damu mbichi na maelezo kuwa ni mtuhumiwa wa ujambazia aliyepigwa risasi na polisi akitaka kuiba kwenye ATM maeneo ya Kilo Road, Dar es Salaam.

Sauti hii hapa chini inayotajwa kuwa ni ya polisi waliohusika na mkasa huo inamueleza marehemu kuwa ni ‘gaidi’, ambapo msemaji anarejelea mavazi na muenekano wa aliyeuawa kama kigezo cha ugaidi wake.

https://soundcloud.com/mohammed-k-ghassani/sikiliza-maelezo-ya-polisi-juu

Baadhi ya magazeti ya leo yameiandika pia stori hiyo kwa kichwa cha habari kinachomtaja kuwa ni “jambazi”, lakini Zanzibar Daima imetumiwa mazungumzo mengine kwa njia ya simu baina ya ndugu na jamaa wa marehemu huyo, ambayo sio tu yanatilia mashaka maelezo hayo ya awali, bali pia yanajenga khofu ya mauaji ya kiholela kufanywa kwa visingizio vya kupambana na ujambazi.

https://soundcloud.com/mohammed-k-ghassani/utata-wa-aliyeuawa-na-polisi

Hapana shaka, mamlaka husika zinapaswa kulifanyia uchunguzi suala hili. Maswali ni mengi kuliko majibu yanayotoka hadi sasa.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.