Mmojawapo miongoni mwa washairi maarufu wa Tanzania, Khamis Amani Nyamaume (1926-1971), katika shairi lake labeti nne, liitwalo ‘Saa’, alitunga akasema: Saa za huku na huko, zimekosana majira Sababu ni mzunguko, haufuati duara Sasa rai iliyoko, ni kubadilisha dira Saa zatupa majira, mafundi zitengezeni…
